Breaking News

Mtangazaji Salim Kikeke Ala Shavu Zanzibar

 



Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imempa jukumu la kuwa mshauri wa masuala ya habari na uhusiano mtangazaji wa zamani wa BBC Salim Kikeke. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Kikeke ameeleza kuwa jukumu hilo kwake ni kama sehemu ya lengo lake la kurejea nchini kwa kuwa alikuwa nia ya kulisaidia taifa lake.

“Nimerejea Tanzania ili kulisaidia taifa langu kwa hali na mali hii ni fursa ya kipekee kupata nafasi ya kuhusishwa kwenye sera ya uchumi wa bluu ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibae Dk. Hussein Mwinyi.

Hapo awali Kikeke alitabiriwa kuwa ameacha kazi katika Shirika la Utangazaji la Uengereza (BBC) kwa kuwa ameitiwa kazi ya kuwa Msemaji wa Serikali kama ilivyokuwa kwa Zuhura Yunus alipoachaka kazi kwenye shirika hilo hilo la BBC na Serikali ya Tanzania kumteua kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu .

Uvumi huu ulipata nguvu baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumuondoa kwenye nafasi ya usemaji wa Serikali Gerson Msigwa na kumfanya kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo lakini uvumi huu ulikwisha pale alipoteuliwa Mobhare Matinyi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke kushika nafasi ya msemaji wa Serikali.

Kwa Kikeke aliyetabiriwa kushika nafasi ya kulitumikia taifa sasa amekuwa mshauri wa masuala ya habari ZIPA.




0 Comments

Advertisement
Advertisement
Advertisement
Advertisement

Type and hit Enter to search

Close